Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 10:1-4

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Yesu Awatuma Wale Kumi Na Wawili

1 Ndipo Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, naye akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, ili waweze kuwatoa na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila aina.

2 Haya ndiyo majina ya hao mitume kumi na wawili: wa kwanza, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye; Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye; 3 Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo; 4 Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote aliyemsaliti Yesu.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Ndipo Isa akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, naye akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, ili waweze kuwatoa na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila aina.

    2 Haya ndiyo majina ya hao mitume kumi na wawili:

    wa kwanza, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye;

    Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye;

    3 Filipo, na Bartholomayo;

    Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru;

    Yakobo mwana wa Alfayo, na Thadayo;

    4 Simoni Mkananayo10:4 yaani Mzelote; Wazelote walikuwa kikundi cha Kiyahudi wenye imani kali waliompinga Kaisari na utawala wa Rumi., na Yuda Iskariote aliyemsaliti Isa.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Mk 6:7-13;Lk 9:1-5Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.

    2 Mk 3:14-19;Lk 6:13-16;Yn 1:40-49Na majina ya hao mitume kumi na wawili ni haya; Wa kwanza Simoni aliyeitwa Petro, na Andrea nduguye; Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye; 3 Filipo, na Bartholomayo; Tomaso, na Mathayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo, na Thadayo; 4 Simoni Mkananayo, na Yuda Iskarioti, naye ndiye aliyemsaliti.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.