Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 12:46-50

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

46 Wakati alikuwa angali anazungumza na makutano, mama yake na ndugu zake wakasimama nje wakitaka kuongea naye. 47 Ndipo mtu mmoja akamwambia, "Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kuongea na wewe."

48 Lakini yeye akamjibu na kumwambia yule mtu, "Mama yangu ni nani, nao ndugu zangu ni nani?" 49 Akawanyooshea mkono wanafunzi wake, akasema, "Hawa hapa ndio mama yangu na ndugu zangu! 50 Kwa maana yeyote afanyaye mapenzi ya Baba yangu wa mbinguni, huyo ndiye ndugu yangu, na dada yangu na mama yangu."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    46 Wakati alikuwa angali anazungumza na umati wa watu, mama yake na ndugu zake wakasimama nje wakitaka kuongea naye. 47 Ndipo mtu mmoja akamwambia, "Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kuongea na wewe."

    48 Lakini yeye akamjibu na kumwambia yule mtu, "Mama yangu ni nani, nao ndugu zangu ni nani?" 49 Akawanyooshea mkono wanafunzi wake, akasema, "Hawa hapa ndio mama yangu na ndugu zangu! 50 Kwa maana yeyote afanyaye mapenzi ya Baba12:50 Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. yangu wa mbinguni, huyo ndiye kaka yangu, na dada yangu, na mama yangu."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    46 Mk 3:31-35;Lk 8:19-21Alipokuwa katika kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wataka kusema naye.Mt 13:5547 Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe. 48 Lk 2:49Akajibu, akamwambia yule aliyempasha habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani? 49 Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu! 50 Rum 8:29;Yn 15:14Kwa maana yeyote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye kaka yangu, na dada yangu na mama yangu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.