13 Hii ndiyo sababu nasema nao kwa mifano:
"Ingawa wanatazama, hawaoni;
wanasikiliza, lakini hawasikii, wala hawaelewi.
14 Kwao unatimia ule unabii wa Isaya aliposema:
" ‘Hakika mtasikiliza lakini hamtaelewa;
na pia mtatazama lakini hamtaona.
15 Kwa kuwa mioyo ya watu hawa imekuwa migumu;
hawasikii kwa masikio yao,
na wamefumba macho yao.
Wasije wakaona kwa macho yao,
na wakasikiliza kwa masikio yao,
wakaelewa kwa mioyo yao,
na kugeuka nami nikawaponya.’