Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 14

15 Ilipofika jioni, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, "Mahali hapa ni nyikani, na muda sasa umekwisha. Waage makutano ili waende zao vijijini wakajinunulie chakula."

16 Yesu akawaambia, "Hakuna sababu ya wao kuondoka. Ninyi wapeni chakula."

17 Wakamjibu, "Tuna mikate mitano na samaki wawili tu."

18 Akawaambia, "Nileteeni hivyo vitu hapa." 19 Yesu akaagiza makutano wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakawagawia makutano. 20 Wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili. 21 Idadi ya watu waliokula walikuwa wanaume wapatao 5,000, bila kuhesabu wanawake na watoto.

Veja também