28 Petro akamjibu, "Bwana, ikiwa ni wewe, niambie nije kwako nikitembea juu ya maji."
29 Yesu akamwambia, "Njoo."
Basi Petro akatoka kwenye chombo, akatembea juu ya maji kumwelekea Yesu. 30 Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama, huku akipiga kelele, "Bwana, niokoe!"
31 Mara Yesu akaunyoosha mkono wake na kumshika, akamwambia, "Wewe mwenye imani haba, kwa nini uliona shaka?"