Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 16:13,16,21-24,28

13 Basi Yesu alipofika katika eneo la Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake, "Watu husema kwamba mimi Mwana wa Adamu ni nani?"

16 Simoni Petro akamjibu, "Wewe ndiwe Kristo,16:16 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Mwana wa Mungu aliye hai."

21 Tangu wakati huo, Yesu alianza kuwaeleza wanafunzi wake kwamba hana budi kwenda Yerusalemu na kupata mateso mengi mikononi mwa wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa sheria, na kwamba itampasa auawe lakini siku ya tatu kufufuliwa.

22 Petro akamchukua kando, akaanza kumkemea akisema, "Haiwezekani, Bwana! Jambo hili kamwe halitakupata!"

23 Lakini Yesu akageuka na kumwambia Petro, "Rudi nyuma yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu."

24 Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate. 28 Nawaambia kweli, baadhi yenu hapa hawataonja mauti kabla ya kumwona Mwana wa Adamu akija katika Ufalme wake."

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.