15 Akawauliza, "Je, ninyi mnasema mimi ni nani?"
16 Simoni Petro akamjibu, "Wewe ndiwe Kristo,16:16 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Mwana wa Mungu aliye hai."
17 Naye Yesu akamwambia, "Heri wewe, Simoni Bar-Yona,16:17 Bar-Yona ni neno la Kiaramu, maana yake ni Mwana wa Yona. kwa maana hili halikufunuliwa kwako na mwanadamu, bali na Baba yangu aliye mbinguni.