Pular para o conteúdo
Publicidade

Mateus 16

Chachu Ya Mafarisayo Na Masadukayo

5 Wanafunzi wake walipofika ngʼambo ya bahari, walikuwa wamesahau kuchukua mikate. 6 Yesu akawaambia, "Jihadharini. Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo."

7 Wakajadiliana wao kwa wao, wakisema, "Ni kwa sababu hatukuleta mikate."

8 Yesu, akifahamu majadiliano yao, akauliza, "Enyi wa imani haba! Mbona mnajadiliana miongoni mwenu kuhusu kutokuwa na mikate? 9 Je, bado hamwelewi? Je, hamkumbuki ile mikate mitano iliyolisha watu 5,000 na idadi ya vikapu vingapi vya mabaki mlivyokusanya? 10 Au ile mikate saba iliyolisha watu 4,000 na idadi ya vikapu vingapi vya mabaki mlivyokusanya? 11 Inakuwaje mnashindwa kuelewa kwamba nilikuwa sisemi nanyi habari za mikate? Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo." 12 Ndipo wakaelewa kwamba alikuwa hasemi juu ya chachu ya kutengeneza mikate, bali juu ya mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.

Veja também