Publicidade

Mateus 17

Yesu Na Petro Watoa Kodi Ya Hekalu

24 Baada ya Yesu na wanafunzi wake kufika Kapernaumu, wakusanya kodi ya Hekalu17:24 Kodi ya Hekalu ilikuwa didrachmas, yaani drakma mbili, ambazo ni sawa na nusu shekeli. wakamjia Petro na kumuuliza, "Je, Mwalimu wenu halipi kodi ya Hekalu?"

25 Petro akajibu, "Ndiyo, yeye hulipa." Petro aliporudi nyumbani, Yesu akawa wa kwanza kulizungumzia, akamuuliza, "Unaonaje Simoni? Wafalme wa dunia hupokea ushuru na kodi kutoka kwa nani? Je, ni kutoka kwa watoto wao au kutoka kwa watu wengine?"

26 Petro akamjibu, "Kutoka kwa watu wengine." Yesu akamwambia, "Kwa hiyo watoto wao wamesamehewa. 27 Lakini ili tusije tukawaudhi, nenda baharini ukatupe ndoana. Mchukue samaki wa kwanza utakayemvua. Fungua kinywa chake nawe utakuta humo fedha, ichukue ukalipe kodi yako na yangu."

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-