Aliye Mkuu Katika Ufalme Wa Mbinguni
1 Wakati huo, wanafunzi wakamjia Yesu na kumuuliza, "Je, nani aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni?"
2 Yesu akamwita mtoto mdogo na kumsimamisha katikati yao. 3 Naye akasema: "Amin, nawaambia, msipookoka na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni. 4 Kwa hiyo mtu yeyote anyenyekeaye kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni.