Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 18:1-5,10

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

Aliye Mkuu Katika Ufalme Wa Mbinguni

1 Wakati huo, wanafunzi wakamjia Yesu na kumuuliza, "Je, nani aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni?"

2 Yesu akamwita mtoto mdogo na kumsimamisha katikati yao. 3 Naye akasema: "Amin, nawaambia, msipookoka na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni. 4 Kwa hiyo mtu yeyote anyenyekeaye kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni.

5 "Yeyote amkaribishaye mtoto mdogo kama huyu kwa Jina langu, anikaribisha mimi.

10 "Angalia ili usimdharau mmojawapo wa hawa wadogo, kwa maana nawaambia, malaika wao mbinguni daima wanauona uso wa Baba yangu aliye mbinguni. [

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Wakati huo, wanafunzi wakamjia Isa na kumuuliza, "Je, nani aliye mkuu kuliko wote katika ufalme wa mbinguni?"

    2 Isa akamwita mtoto mdogo na kumsimamisha katikati yao. 3 Naye akasema: "Amin, nawaambia, msipoongoka na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika ufalme wa mbinguni. 4 Kwa hiyo mtu yeyote anyenyekeaye kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika ufalme wa mbinguni.

    5 "Yeyote amkaribishaye mtoto mdogo kama huyu kwa Jina langu, anikaribisha mimi.

    10 "Chungeni ili msimdharau mmoja wa hawa wadogo. Kwa maana nawaambia, malaika wao mbinguni daima wanauona uso wa Baba18:10 Jina Baba linaonesha uhusiano maalum wa Isa na Mwenyezi Mungu. yangu aliye mbinguni. [

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    1 Lk 22:24Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakisema,Mk 9:33-47;Lk 9:46-482 Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao, 3 Mk 10:15;Lk 18:17;Mt 19:14;Yn 3:3-5akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama watoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.

    4 Basi, yeyote ajinyenyekezaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni. 5 Mt 10:40;Yn 13:20Na yeyote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi;

    10 Ebr 1:14Angalieni msidharau mmojawapo wa wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni. [

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.