Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 20

Ombi La Mama Yake Yakobo Na Yohana

20 Kisha mama yao wana wa Zebedayo akamjia Yesu pamoja na wanawe, naye akapiga magoti mbele yake, akamwomba Yesu amfanyie jambo fulani.

21 Yesu akamuuliza, "Unataka nini?" Akajibu, "Tafadhali, wajalie wanangu hawa ili mmoja aketi upande wako wa kuume, na mwingine upande wako wa kushoto katika Ufalme wako."

22 Yesu akawaambia, "Ninyi hamjui mnaloliomba. Je, mnaweza kukinywea kikombe nitakachonywea mimi?"

Wakajibu, "Tunaweza."

23 Yesu akawaambia, "Kwa kweli kikombe changu mtakinywea, lakini kuketi upande wangu wa kuume au wa kushoto si langu mimi kuwapa. Nafasi hizo ni za wale ambao wameandaliwa na Baba yangu."

Veja também