Yesu Awashutumu Walimu Wa Sheria Na Mafarisayo
1 Kisha Yesu akauambia umati wa watu pamoja na wanafunzi wake: 2 "Walimu wa sheria na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Mose, 3 hivyo inawapasa kuwatii na kufanya kila kitu wanachowaambia. Lakini msifuate yale wanayotenda, kwa sababu hawatendi yale wanayohubiri. 4 Wao hufunga mizigo mikubwa na kuiweka mabegani mwa watu, lakini wao wenyewe hawako radhi hata kuinua kidole ili kuisogeza.
5 "Wao hutenda mambo yao yote ili waonekane na watu. Hupanua vikasha vyao vyenye maandiko ya sheria na kurefusha matamvua ya mavazi yao. 6 Wanapenda kukalia viti vya heshima katika karamu, na vile viti maalum sana katika masinagogi. 7 Hupenda kusalimiwa masokoni na kutaka watu wawaite ‘Rabi.’23:7 Rabi maana yake Bwana, Mwalimu.