4 Yesu akawajibu, "Jihadharini, mtu yeyote asiwadanganye. 5 Kwa maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye Kristo,’24:5 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. nao watawadanganya wengi. 6 Mtasikia habari za vita na matetesi ya vita. Angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia. Lakini ule mwisho bado. 7 Taifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali. 8 Haya yote yatakuwa ndio mwanzo wa utungu.
Mathayo 24:4-8
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
4 Isa akawajibu, "Jihadharini, mtu yeyote asiwadanganye. 5 Kwa maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye Al-Masihi24:5 Al-Masihi maana yake Aliyetiwa mafuta.,’ nao watawadanganya wengi. 6 Mtasikia habari za vita na tetesi za vita. Angalieni msitishike, kwa maana haya hayana budi kutukia. Lakini ule mwisho bado. 7 Taifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali. 8 Haya yote yatakuwa ndio mwanzo wa uchungu.
- SRUV Swahili Revised Union Version
4 Yesu akajibu, akawaambia, Angalieni, mtu asiwadanganye. 5 Mt 24:24;Yn 5:43;Mdo 5:36,37;1 Yoh 2:18Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, Mimi ni Kristo; nao watadanganya wengi. 6 Dan 2:28Nanyi mtasikia habari za vita na tetesi za vita; angalieni, msitishwe; maana hayo hayana budi kutukia; lakini ule mwisho bado. 7 Isa 19:2;2 Nya 15:6Kwa maana taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na mitetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali. 8 Hayo yote ndiyo mwanzo wa uchungu.
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.