Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 3:13-17

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

13 Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Mto Yordani ili Yohana ambatize. 14 Lakini Yohana akajitahidi kumzuia, akimwambia, "Mimi ninahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu nikubatize?"

15 Lakini Yesu akamjibu, "Kubali hivi sasa, kwa maana ndivyo itupasavyo kwa njia hii kuitimiza haki yote." Hivyo Yohana akakubali.

16 Naye Yesu alipokwisha kubatizwa, mara alipotoka ndani ya maji, ghafula mbingu zikafunguka, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua na kutulia juu yake. 17 Nayo sauti kutoka mbinguni ikasema, "Huyu ni Mwanangu mpendwa, ambaye ninapendezwa sana naye."

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    13 Kisha Isa akaja kutoka Galilaya hadi Mto Yordani ili Yahya ambatize. 14 Lakini Yahya akajitahidi kumzuia, akimwambia, "Mimi ninahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu nikubatize?"

    15 Lakini Isa akamjibu, "Kubali hivi sasa, kwa maana ndivyo itupasavyo kwa njia hii kuitimiza haki yote." Hivyo Yahya akakubali.

    16 Naye Isa alipokwisha kubatizwa, mara alipotoka ndani ya maji, ghafula mbingu zikafunguka, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua na kutulia juu yake. 17 Nayo sauti kutoka mbinguni ikasema, "Huyu ni Mwanangu mpendwa; ninapendezwa sana naye."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    13 Mk 1:9-11;Lk 3:21-22;Yn 1:31-34Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. 14 Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? 15 Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Ndipo akakubali. 16 Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara aliibuka kutoka majini na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, na kutua juu yake; 17 Mwa 22:2;Zab 2:7;Isa 42:1;Mt 12:18;17:5;Mk 1:11;Lk 9:35na tazama, sauti kutoka mbinguni ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.