Mwanamke Aponywa
18 Yesu alipokuwa akiwaambia mambo haya, mara akaingia kiongozi wa sinagogi akapiga magoti mbele yake, akamwambia, "Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini njoo uweke mkono wako juu yake, naye atakuwa hai." 19 Yesu akaondoka akafuatana naye, nao wanafunzi wake pia wakaandamana naye.