Pular para o conteúdo
Publicidade

Mathayo 9:9-13

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

9 Yesu alipokuwa akienda kutoka huko, alimwona mtu mmoja jina lake Mathayo akiwa ameketi forodhani mahali pa kutoza ushuru. Yesu akamwambia, "Nifuate." Mathayo akaondoka, akamfuata.

10 Yesu alipokuwa akila chakula ndani ya nyumba ya Mathayo, watoza ushuru wengi na "wenye dhambi" wakaja kula pamoja naye na wanafunzi wake. 11 Mafarisayo walipoona mambo haya, wakawauliza wanafunzi wake, "Kwa nini Mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na ‘wenye dhambi’?"

12 Lakini Yesu aliposikia hayo, akawaambia, "Watu wenye afya hawahitaji tabibu, lakini wale walio wagonjwa ndio wanaohitaji tabibu. 13 Nendeni mkajifunze maana ya maneno haya: ‘Nataka rehema, wala si dhabihu.’ Kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi."

Yesu Aulizwa Kuhusu Kufunga

(Marko 2:18-22; Luka 5:33-39)

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    9 Isa alipokuwa akienda kutoka huko, alimwona mtu mmoja jina lake Mathayo akiwa ameketi forodhani mahali pa kutoza ushuru. Isa akamwambia, "Nifuate." Mathayo akasimama, akamfuata.

    10 Isa alipokuwa ameketi akila chakula ndani ya nyumba ya Mathayo, watoza ushuru wengi na wenye dhambi wakaja, wakaketi kula pamoja naye na wanafunzi wake. 11 Mafarisayo9:11 Kundi la kidini la Wayahudi; walifuata Torati kwa dhati, hasa maagizo kuhusu utakaso. Pia waliamini katika malaika, ufufuo wa wafu, na kuja kwa Masihi ambaye atarejesha ufalme wa Daudi na ukuu wa taifa la Israeli. walipoona mambo haya, wakawauliza wanafunzi wake, "Kwa nini Mwalimu wenu anakula na watoza ushuru na wenye dhambi?"

    12 Lakini Isa aliposikia hayo, akawaambia, "Watu wenye afya hawahitaji tabibu, lakini wale walio wagonjwa ndio wanaohitaji tabibu. 13 Nendeni mkajifunze maana ya maneno haya: ‘Nataka rehema, wala si dhabihu.’ Kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi."

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    9 Mk 2:13-17;Lk 5:27-32Naye Yesu alipokuwa akipita kutoka huko aliona mtu ameketi forodhani, aitwaye Mathayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata. 10 Lk 15:1-2Ikawa alipoketi nyumbani ale chakula, tazama, watoza ushuru wengi na wenye dhambi walikuja wakaketi pamoja na Yesu na wanafunzi wake. 11 Mafarisayo walipoona, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi? 12 Naye aliposikia, aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa. 13 Mt 12:7;Hos 6:6;1 Sam 15:22;18:11Lakini nendeni, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka; kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.