Wito Wa Hekima
1 Je, hekima haitani?
Je, ufahamu hapazi sauti?
10 Chagua mafundisho yangu badala ya fedha,
maarifa badala ya dhahabu safi,
11 kwa maana hekima ina thamani kuliko marijani
na hakuna chochote unachohitaji kinacholingana naye.
12 "Mimi hekima, nakaa pamoja na busara;
ninamiliki maarifa na busara.
13 Kumcha Bwana ni kuchukia uovu;
ninachukia kiburi na majivuno,
tabia mbaya na mazungumzo potovu.
32 "Basi sasa wanangu, nisikilizeni;
heri wale wanaozishika njia zangu.
33 Sikilizeni mafundisho yangu mwe na hekima;
msiyapuuze.
34 Heri mtu yule anisikilizaye mimi,
akisubiri siku zote malangoni mwangu,
akingoja kwenye vizingiti vya mlango wangu.
35 Kwa maana yeyote anipataye mimi amepata uzima
na kujipatia kibali kutoka kwa Bwana.
36 Lakini yeyote ashindwaye kunipata
hujiumiza mwenyewe;
na wote wanichukiao mimi hupenda mauti."