Makaribisho Ya Hekima Na Ya Upumbavu
1 Hekima amejenga nyumba yake;
amechonga nguzo zake saba.
2 Ameandaa nyama na kuchanganya divai yake;
pia ameandaa meza yake.
3 Amewatuma watumishi wake wa kike, naye huita
kutoka mahali pa juu sana pa mji.
4 Anawaambia wale wasio na akili,
"Wote ambao ni wajinga na waje hapa!
5 Njooni, mle chakula changu
na mnywe divai niliyoichanganya.
6 Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi;
tembeeni katika njia ya ufahamu.
10 "Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,
na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.