Pular para o conteúdo
Publicidade

Warumi 10:14-17

ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

14 Lakini watamwitaje yeye ambaye hawajamwamini? Nao watawezaje kumwamini yeye ambaye hawajamsikia? Tena watamsikiaje bila mtu kuwahubiria? 15 Nao watahubirije wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, "Tazama jinsi ilivyo mizuri miguu yao wale wanaohubiri habari njema!"

16 Lakini si wote waliotii Habari Njema. Kwa maana Isaya asema, "Bwana, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?" 17 Basi, imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    14 Lakini watamwitaje yeye ambaye hawajamwamini? Nao watawezaje kumwamini yeye ambaye hawajamsikia? Tena watamsikiaje bila mtu kuwahubiria? 15 Nao watahubirije wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, "Tazama jinsi ilivyo mizuri miguu yao wale wanaohubiri Habari Njema!"

    16 Lakini si wote waliotii Injili. Kwa maana Isaya asema, "Mwenyezi Mungu, ni nani aliyeamini ujumbe wetu?" 17 Basi, imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Al-Masihi.

  2. SRUV Swahili Revised Union Version

    14 Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? 15 Isa 52:7Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!

    16 Isa 43:1Lakini si wote walioitii ile Habari Njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, ni nani aliyeziamini habari zetu? 17 Yn 17:20Basi imani, hutokana na kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.