Pular para o conteúdo
Publicidade

Ruthu 1:1,3,5,8,14,16,17,20,21

Naomi Na Ruthu

1 Wakati Waamuzi walipotawala Israeli, kulikuwa na njaa katika nchi. Mtu mmoja kutoka nchi ya Bethlehemu ya Yuda, pamoja na mke wake na wanawe wawili, akaenda kuishi katika nchi ya Moabu.

3 Elimeleki mumewe Naomi akafa, hivyo Naomi akabaki na wanawe wawili. 5 Maloni na Kilioni pia wakafa. Basi Naomi akabaki hana mume wala wanawe wawili.

8 Ndipo Naomi akawaambia wale wakwe zake wawili, "Rudini, kila mmoja wenu nyumbani kwa mama yake. Bwana na awatendee fadhili kama mlivyowatendea hao waliofariki, na pia mimi.

14 Kisha wakalia tena kwa sauti. Orpa akambusu mama mkwe wake, akaenda zake, lakini Ruthu akaambatana naye.

16 Lakini Ruthu akajibu, "Usinisihi nikuache au niache kukufuata. Utakakokwenda nami nitakwenda, na wewe utakapoishi nitaishi. Watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako atakuwa Mungu wangu. 17 Pale utakapofia nami nitafia hapo, na papo hapo nitazikwa. Bwana na aniadhibu vikali, kama kitu kingine chochote kitanitenga nawe isipokuwa kifo."

20 Akawaambia, "Msiniite tena Naomi,1:20 Naomi maana yake Wa Kupendeza, Wa Kufurahisha. niiteni Mara,1:20 Mara maana yake Chungu. kwa sababu Mwenyezi1:20 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania. amenitendea mambo machungu sana. 21 Mimi niliondoka hali nimejaa, lakini Bwana amenirudisha mtupu. Kwa nini kuniita Naomi? Bwana amenitendea mambo machungu; Mwenyezi ameniletea msiba."

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Rute
Ver todos os capítulos de Rute