Pular para o conteúdo
Publicidade

Ruthu 4:1,2,6,7,9,10,12,13,17

Boazi Amwoa Ruthu

1 Boazi akakwea mpaka kwenye lango la mji, akaketi pale. Yule mtu wa jamaa aliyekuwa wa karibu wa kukomboa, ambaye Boazi alimtaja, akaja. Boazi akasema, "Njoo hapa, rafiki yangu. Karibu uketi." Naye akakaribia, akaketi.

2 Boazi akatwaa watu kumi miongoni mwa wazee wa mji, akawaambia, "Ketini hapa." Nao wakaketi.

6 Aliposikia hili, yule jamaa wa karibu wa kukomboa akasema, "Basi mimi sitaweza kuikomboa, kwa sababu inaonekana nitauhatarisha urithi wangu. Wewe ikomboe mwenyewe. Mimi sitaweza."

7 (Basi katika siku za kale huko Israeli, ili kukamilisha tendo la kukomboa na kukabidhiana mali, mmoja huvua kiatu chake na kumpatia mwingine. Hii ilikuwa ni njia ya kuhalalisha mabadilishano katika Israeli.)

9 Kisha Boazi akawatangazia wazee na watu wote waliokuwepo, "Leo ninyi ni mashahidi kwamba mimi nimenunua kutoka kwa Naomi yote yaliyokuwa mali ya Elimeleki, Kilioni na Maloni. 10 Nimemchukua pia Ruthu, Mmoabu, mjane wa Maloni, awe mke wangu, ili kuendeleza jina la marehemu pamoja na mali zake, ili jina lake marehemu lisitoweke miongoni mwa jamaa yake, wala katika kumbukumbu za mji wake. Leo hivi ninyi ni mashahidi!"

12 Kupitia kwa watoto ambao Bwana atakupa kutokana na huyu mwanamwali, jamaa yako na ifanane na ya Peresi, ambaye Tamari alimzalia Yuda."

Wazao Wa Boazi

13 Basi Boazi akamwoa Ruthu, naye akawa mke wake. Alipoingia kwake, Bwana akamjalia Ruthu, naye akapata mimba, akamzaa mtoto wa kiume.

17 Wanawake waliokuwa jirani zake wakasema, "Naomi ana mtoto wa kiume." Wakamwita jina lake Obedi. Yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Rute
Ver todos os capítulos de Rute