Pular para o conteúdo
Publicidade

Rute 4

14 Wanawake wakamwambia Naomi: "Ahimidiwe Bwana, asiyekuacha bila kuwa na jamaa wa karibu wa kukomboa. Na awe mashuhuri katika Israeli yote! 15 Atakurejeshea uhai wako na kukuangalia katika siku za uzee wako. Kwa maana mkweo ambaye anakupenda, na ambaye kwako ni bora zaidi ya watoto wa kiume saba, ndiye alimzaa."

16 Basi Naomi akamchukua yule mtoto, akampakata na akawa mlezi wake. 17 Wanawake waliokuwa jirani zake wakasema, "Naomi ana mtoto wa kiume." Wakamwita jina lake Obedi. Yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi.

Veja também

Rute
Ver todos os capítulos de Rute