3 Yehoshafati akaogopa, akaamua kumtafuta Mwenyezi Mungu, na akatangaza kwa Yuda wote kufunga. 4 Watu wa Yuda wakakusanyika pamoja ili kutafuta msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Wakaja kutoka kila mji wa Yuda ili kumtafuta.
15 Akasema: "Sikilizeni, enyi Yuda wote nanyi nyote mnaoishi Yerusalemu, nawe Mfalme Yehoshafati! Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kwenu, ‘Msiogope wala msifadhaike kwa sababu ya jeshi hili kubwa. Kwa maana vita hivi si vyenu, bali ni vya Mungu. 17 Hamtahitaji kupigana vita hivi. Kaeni kwenye nafasi zenu, simameni imara na mkaone wokovu Mwenyezi Mungu atakaowapatia, enyi Yuda na Yerusalemu. Msiogope, wala msifadhaike. Kesho tokeni mwende mkawakabili, naye Mwenyezi Mungu atakuwa pamoja nanyi.’ "
22 Walipoanza kuimba na kusifu, Mwenyezi Mungu akaweka waviziaji dhidi ya watu wa Amoni, Moabu na wale wa Mlima Seiri waliokuwa wamekuja kuishambulia Yuda, nao wakashindwa.