24 naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. 25 Kut 24:6-8;Yer 31:31-34;Zek 9:11Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. 26 Mt 26:29Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.
Kula chakula cha Bwana isivyostahili
27 Ebr 6:6;10:29Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana. 28 Mt 26:22;2 Kor 13:5Lakini mtu ajihoji mwenyewe, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe.