3 Isa 53:5-12Kwa maana niliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo Maandiko; 4 Zab 16:8-10;Mt 12:40;Mdo 2:24-32;2 Fal 20:5;Isa 54:7;Hos 6:2;Yon 1:17na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo Maandiko; 5 Mt 28:16-17;Mk 16:14;Lk 24:34,36;Yn 20:19na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Kumi na Wawili; 6 baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala; 7 Lk 24:50baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote; 8 Mdo 9:3-6;1 Kor 9:1na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake.
1 Wakorintho 15:3-8
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
3 Kwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: Kwamba Al-Masihi alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama Maandiko yanavyosema, 4 ya kuwa alizikwa na alifufuliwa siku ya tatu, kama Maandiko yanavyosema, 5 na kwamba alimtokea Kefa15:5 yaani Petro, kisha akawatokea wale kumi na wawili. 6 Baadaye akawatokea wale ndugu waumini zaidi ya mia tano kwa pamoja, ambao wengi wao bado wako hai, ingawa wengine wamelala. 7 Ndipo akamtokea Yakobo na kisha mitume wote. 8 Mwisho wa wote, akanitokea mimi pia, ambaye ni kama aliyezaliwa si kwa wakati wake.
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
3 Kwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: Kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yasemavyo Maandiko, 4 ya kuwa alizikwa na alifufuliwa siku ya tatu, kama yasemavyo Maandiko, 5 na kwamba alimtokea Kefa,15:5 Yaani Petro. kisha akawatokea wale kumi na wawili. 6 Baadaye akawatokea wale ndugu waumini zaidi ya 500 kwa pamoja, ambao wengi wao bado wako hai, ingawa wengine wamelala. 7 Ndipo akamtokea Yakobo na kisha mitume wote. 8 Mwisho wa wote, akanitokea mimi pia, ambaye ni kama aliyezaliwa si kwa wakati wake.
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.