Publicidade

1 Coríntios 6

Mashitaka miongoni mwa waumini

1 Je! Mmoja wenu akiwa ana shtaka juu ya mwenzake athubutuje kushitaki mbele ya wasio haki, wala si mbele ya watakatifu? 2 Ufu 3:21;Dan 7:22 Au hamjui ya kwamba watakatifu watauhukumu ulimwengu? Na ikiwa ulimwengu utahukumiwa na ninyi, je! Hamstahili kukata hukumu zilizo ndogo? 3 Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya? 4 Basi, mkiwa na mahali panapohukumiwa mambo ya maisha haya, mwawaweka kuwa waamuzi hao waliohesabiwa kuwa si kitu; katika kanisa? 5 Nasema hayo nipate kuwatahayarisha. Je! Ndivyo, kwamba kwenu hakuna hata mtu mmoja mwenye hekima, awezaye kukata maneno ya ndugu zake? 6 Bali mwashitakiana, ndugu kwa ndugu, tena mbele yao wasioamini. 7 Mt 5:39;1 The 5:15;1 Pet 3:9 Basi imekuwa upungufu kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyang’anywa mali zenu? 8 Bali kinyume cha hayo ninyi wenyewe mwadhulumu watu na kunyang’anya mali zao; naam, hata za ndugu zenu. 9 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, 10 Gal 5:19-21 wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi. 11 Tit 3:3-7 Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu.

Mtukuze Mungu katika mwili na Roho

12 1 Kor 10:23 Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu chochote. 13 1 The 4:3-5 Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili. 14 1 Kor 15:15,20;2 Kor 4:14;Rum 8:11 Naye Mungu alimfufua Bwana, na tena atatufufua sisi kwa uweza wake. 15 1 Kor 12:27 Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? La hasha! 16 Mwa 2:24 Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. 17 Yn 17:21,22;Efe 5:30;2 Kor 3:17 Lakini yeye aliyeungwa na Bwana ni roho moja naye. 18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. 19 1 Kor 3:16;2 Kor 6:16 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; 20 1 Pet 1:18,19;1 Kor 7:23;Flp 1:20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_12-11-46-