16 Yn 13:1;15:13;Gal 2:20Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. 17 1 Yoh 4:20;Kum 15:7Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? 18 Yak 1:22;2:15,16Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.