10 1 Yoh 2:2Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. 11 Mt 18:33Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. 12 Yn 1:18Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.