6 1 Pet 5:10;Ebr 12:11;Yak 1:2;2 Kor 4:17Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa muda mfupi, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; 7 Mit 17:3;Mal 3:3;Rum 2:7,10;Yak 1:3ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo. 8 Yn 17:20;20:29;2 Kor 5:7;2 Tim 4:8Naye mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamumwoni sasa, mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu, 9 Rum 6:22katika kuupokea mwisho wa imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu.