Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Petro 2:13-17

SRUV Swahili Revised Union Version

13 Rum 13:1-7;Tit 3:1Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; iwe ni mfalme kama mwenye cheo kikubwa; 14 au iwe ni watawala, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema. 15 1 Pet 3:16Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu; 16 Gal 5:13kama walio huru, ila wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu. 17 Rum 12:10;Mit 24:21;Mt 22:21Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    13 Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, tiini kila mamlaka iliyowekwa na wanadamu: Awe ni mfalme kwani ndiye aliye na mamlaka ya juu zaidi, 14 au wawe maafisa aliowaweka. Kwa kuwa mfalme amewatuma ili kuwaadhibu wale wanaokosa, na kuwapongeza wale wanaotenda mema. 15 Kwa maana ni mapenzi ya Mungu kwamba kwa kutenda mema myanyamazishe maneno ya kijinga ya watu wapumbavu. 16 Ishini kama watu huru, lakini msitumie uhuru wenu kama kisingizio cha kutenda uovu, bali ishini kama watumishi wa Mungu. 17 Mheshimuni kila mtu ipasavyo, wapendeni waumini wote, mcheni Mungu, mpeni heshima mfalme.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    13 Kwa ajili ya Bwana, tiini kila mamlaka iliyowekwa na wanadamu: Kwa mfalme kwani ndiye aliye na mamlaka ya juu zaidi, 14 au kwa maafisa aliowaweka, kwa kuwa mfalme amewatuma ili kuwaadhibu wale wanaokosa, na kuwapongeza wale watendao mema. 15 Kwa maana ni mapenzi ya Mungu kwamba kwa kutenda mema mnyamazishe maneno ya kijinga ya watu wapumbavu. 16 Ishini kama watu huru, lakini msitumie uhuru wenu kama kisingizio cha kutenda uovu, bali ishini kama watumishi wa Mungu. 17 Mheshimuni kila mtu ipasavyo: Wapendeni jamaa ya ndugu waumini, mcheni Mungu, mpeni heshima mfalme.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.