21 Mt 16:24;Yn 13:15Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake. 22 Isa 53:9;Yn 8:46;2 Kor 5:21Yeye hakutenda dhambi, wala udanganyifu haukuwapo kinywani mwake. 23 Isa 53:7Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutisha; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki. 24 Isa 53:5,12;1 Yoh 3:5;Rum 6:11;Ebr 9:28Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.