Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Pedro 4

2 1 Yoh 2:16,17Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. 3 Efe 2:2,3;Tit 3:3Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuishi katika uzinzi, tamaa, ulevi, na karamu za kula na kunywa vileo kupindukia, na ibada haramu ya sanamu; 4 mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana. 5 Mdo 10:42;2 Tim 4:1;Rum 14:9,10Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa. 6 1 Pet 3:19;Rum 8:10;1 Kor 5:5Maana kwa ajili hiyo hata hao waliokufa walihubiriwa Injili, ili kwamba wahukumiwe katika mwili kama wahukumiwavyo wanadamu; bali wawe hai katika roho kama Mungu alivyo hai.

7 1 Kor 10:11;1 Yoh 2:18Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala.

Veja também