Kuchunga kundi la Mungu
1 2 Yoh 1:1;3 Yoh 1:1;Rum 8:17;Ufu 1:9Nawasihi wazee walio kwenu, mimi niliye mzee, mwenzi wao, na shahidi wa mateso ya Kristo, na mshirika wa utukufu utakaofunuliwa baadaye; 2 Yn 10:12;21:15-17;Flm 1:14;Tit 1:11;Mdo 20:28;1 Tim 3:2-7lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. 3 2 Kor 1:24;Tit 2:7;Flp 3:17;1 The 1:7Wala si kama wajifanyao mabwana wa wale walio chini ya utunzaji wao, bali iweni mifano kwa lile kundi.