2 Yn 10:12;21:15-17;Flm 1:14;Tit 1:11;Mdo 20:28;1 Tim 3:2-7lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha ya aibu, bali kwa moyo. 3 2 Kor 1:24;Tit 2:7;Flp 3:17;1 The 1:7Wala si kama wajifanyao mabwana wa wale walio chini ya utunzaji wao, bali iweni mifano kwa lile kundi. 5 Mit 3:34;Efe 5:21;Mt 23:12;Yn 13:4,14;Yak 4:6Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.
7 Zab 55:22;Mt 6:25;Flp 4:6huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. 10 1 Pet 1:6;1 The 2:12Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawaimarisha, atawathibitisha, atawatia nguvu na kuwapa msingi imara.