Eliya amkimbia Yezebeli
1 1 Fal 18:40Basi, Ahabu akamwambia Yezebeli habari ya mambo yote aliyoyafanya Eliya, na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga. 2 Rut 1:17;1 Fal 2:23;20:10;2 Fal 6:31;Mit 27:1Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao. 3 Naye alipoona hayo, aliondoka, akaenda aihifadhi roho yake, akafika Beer-sheba, mji wa Yuda, akamwacha mtumishi wake huko.
4 Hes 11:15;Yer 26:14-18;Yon 4:3-8;Flp 1:21-24Lakini yeye mwenyewe akaendelea katika jangwa mwendo wa siku moja, akaenda akaketi chini ya mretemu. Akajiombea roho yake afe, akasema, Yatosha; sasa, Ee BWANA, uiondoe roho yangu; kwa kuwa mimi si mwema kuliko baba zangu. 5 Zab 34:7;Mdo 12:7;Ebr 1:14Naye akajinyosha akalala chini ya mretemu; na tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule. 6 Akatazama, kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake. Akala, akanywa, akajinyosha tena. 7 Malaika wa BWANA akamwendea mara ya pili, akamgusa, akasema, Inuka, ule; maana safari hii ni kubwa mno kwako. 8 Kut 24:18;34:28;Kum 9:9,18;Mt 4:2;Lk 4:2;Kut 3:1Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arubaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.