Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Wafalme 2

Wosia wa Daudi kwa Sulemani

1 Mwa 3:19;47:29;Kum 31:14;2 Sam 14:14;Ayu 30:23;34:15;Zab 89:48;Mhu 12:7Basi siku ya kufa kwake Daudi ikakaribia, akamwusia Sulemani mwanawe, akasema, 2 Yos 23:14;Ebr 9:27Mimi naenda njia ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, ujioneshe kuwa shujaa na hodari; 3 Kum 17:19;29:9;Yos 1:7;1 Nya 22:12,13uyashike mausia ya BWANA, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako; 4 2 Sam 7:25;Zab 132:12;2 Fal 20:3;2 Sam 7:12ili BWANA afanye imara neno lake alilonena kuhusu habari yangu, akisema, Ikiwa watoto wako wataiangalia njia yao, wakienda mbele zangu kwa kweli, kwa moyo wao wote, na kwa roho yao yote, (akasema), hutakosa mtu katika kiti cha enzi cha Israeli.

Veja também