19 Kut 20:12;Law 19:32;Mit 23:22;31:28;Zab 45:9;110:1;Mt 20:21;25:33Basi Bathsheba akaingia kwa mfalme Sulemani, aseme naye kwa ajili ya Adonia. Naye mfalme akainuka kwenda kumlaki, akamwinamia, akaketi katika kiti chake cha enzi; kisha akaagiza awekewe kiti cha enzi mamaye mfalme; naye akaketi mkono wake wa kulia. 20 Ndipo akasema, Haja moja ndogo nakuomba; usinikatalie. Mfalme akamwambia, Omba, mama; kwa kuwa siwezi kukukatalia neno.