5 1 Fal 9:2;2 Nya 1:3;Hes 12:6;Mt 1:20;2:23;Yn 15:7Na huko Gibeoni BWANA akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku; Mungu akamwambia, Omba utakalo nikupe. 6 2 Nya 1:8Sulemani akasema, Umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu, kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na katika unyofu wa moyo pamoja nawe; nawe umemwekea na fadhili hii kubwa, maana umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo. 7 1 Nya 29:1;Mhu 10:16;Yer 1:6;Hes 27:17;Ayu 32:6-8Na sasa, Ee BWANA, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia. 8 Kum 7:6;Mwa 13:16;15:5Na mtumwa wako yuko katikati ya watu wako uliowachagua, watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala kufahamiwa idadi yao, kwa kuwa ni wengi. 9 2 Nya 1:10;Zab 72:1;Mit 2:3;16:16;Yak 1:5;Ebr 5:14Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu watu hawa wako walio wengi?
10 Neno hili likawa jema machoni pa Bwana, ya kuwa Sulemani ameomba neno hili. 11 Yak 4:3Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu; 12 1 Yoh 5:14;1 Fal 4:29;5:12;10:23,24;Mit 3:13-18;8:1-36;Mhu 1:16basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.