Sifa za hekima ya Sulemani
29 Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani. 30 Mwa 25:6;Ayu 28:28;Mit 2:1;Mdo 7:22Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya watu wote4:30 Katika Kiebrania ni wana wote. wa mashariki, na hekima zote za Misri. 31 1 Nya 15:19;6:33Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka. 32 Mit 1:1;Mhu 12:9;Wim 1:1Naye akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano.