10 Ayu 7:11;10:1;Hes 30:3;2 Sam 17:8Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba BWANA akalia sana. 11 Hes 6:5;Mwa 28:20;Hes 21:2;30:3-8;Amu 11:30;Mhu 5:4;Mwa 29:32;Kut 4:31;2 Sam 16:12;Zab 25:18;Mwa 8:1;30:22;Zab 132:1,2Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utayaangalia mateso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto wa kiume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikia kichwani kamwe.