Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Samuel 1

10 Ayu 7:11;10:1;Hes 30:3;2 Sam 17:8Naye huyo mwanamke alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba BWANA akalia sana. 11 Hes 6:5;Mwa 28:20;Hes 21:2;30:3-8;Amu 11:30;Mhu 5:4;Mwa 29:32;Kut 4:31;2 Sam 16:12;Zab 25:18;Mwa 8:1;30:22;Zab 132:1,2Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utayaangalia mateso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto wa kiume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikia kichwani kamwe. 12 Ikawa, hapo alipoendelea kuomba mbele za BWANA, Eli akamwangalia kinywa chake. 13 Basi Hana alikuwa akinena moyoni mwake; midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe; kwa hiyo huyo Eli alimdhania kuwa amelewa. 14 Ndipo Eli akamwambia, Je! Utakuwa mlevi hadi lini? Achilia mbali divai yako. 15 Zab 62:8Hana akajibu, akasema, Hasha! Bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni, mimi sikunywa divai wala kileo, ila nimeimimina roho yangu mbele za BWANA. 16 2 Kor 6:15Usimdhanie mjakazi wako kuwa ni mwanamke asiyefaa kitu; kwa kuwa katika wingi wa kuugua kwangu na kusikitika kwangu ndivyo nilivyonena hata sasa. 17 Amu 18:6;1 Sam 25:35;Lk 7:50;8:48;Zab 20:4,5Ndipo Eli akajibu, akasema, Nenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba. 18 Mwa 33:15;Rut 2:13;Mhu 9:7;Yn 16:24Naye akasema, Mjakazi wako na aone kibali machoni pako. Basi huyo mwanamke akaenda zake, naye akala chakula, wala uso wake haukuhuzunika tena. 19 Mwa 30:22Wakaondoka asubuhi na mapema, wakaomba mbele za BWANA, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye BWANA akamkumbuka. 20 Ikawa, wakati ulipowadia, Hana akachukua mimba na kuzaa mtoto wa kiume; akamwita Samweli, akisema, Kwa kuwa nimemwomba kwa BWANA.

Veja também