Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Samweli 1

22 Lk 2:22;1 Sam 2:11;3:1Bali Hana hakukwea; maana alimwambia mumewe, Sitakwea mimi hata mtoto wangu atakapoachishwa kunyonya, hapo ndipo nitakapomleta, ili awepo mbele za BWANA, akae huko daima. 23 Hes 30:7;2 Sam 7:25Elkana, mumewe, akamwambia, Haya, fanya uonavyo vema; ngoja hadi utakapomwachisha kunyonya; BWANA na alithibitishe neno lake tu. Basi yule mwanamke akangoja, akamnyonyesha mtoto wake, hadi akamwachisha kunyonya. 24 Kum 12:5Naye alipomwachisha kunyonya, akamchukua pamoja naye, na ng’ombe watatu,1:24 Au, ng’ombe wa miaka mitatu. na efa moja ya unga, na chupa ya divai, akamleta nyumbani kwa BWANA, huko Shilo; na yule mtoto alikuwa mtoto mdogo.

Veja também