Sifa za maaskofu
1 Mdo 20:28Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu,3:1 Askofu: maana yake ni, Mwangalizi. atamani kazi njema. 2 Tit 1:6-9Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkarimu, ajuaye kufundisha; 3 asiwe mtu wa kulewa, asiye dhalimu; bali awe mpole; asiwe mbishi, wala asiwe mwenye kupenda fedha; 4 1 Sam 2:12mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; 5 (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje kanisa la Mungu?) 6 Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. 7 1 Tim 5:10;2 Kor 8:21;1 Kor 5:12,13Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.