Maagizo kwa Timotheo na baraka
20 1 Tim 4:7;2 Tim 1:14Ee Timotheo, ilinde hiyo amana; ujiepushe na mazungumzo yasiyo ya kimungu, yasiyo na maana, na mashindano ya elimu iitwayo elimu kwa uongo; 21 1 Tim 1:6;2 Tim 2:18ambayo wengine kwa kuikiri wamepoteza Imani. Neema na iwe pamoja nanyi.