1 Mt 24:36 Lakini, ndugu, kuhusu nyakati na majira, hamna haja niwaandikie. 2 Mt 24:42-44;Ufu 3:3;16:15;Lk 12:39;2 Pet 3:10 Maana ninyi wenyewe mnajua hakika ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwizi ajavyo usiku. 3 Yer 6:14;Yn 16:21,22;Mt 24:39;Lk 21:34,35 Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa. 4 Bali ninyi, ndugu, hamko gizani, hata siku ile iwapate kama mwizi. 5 Rum 13:12;Efe 5:9 Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza. 6 Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi. 7 Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku. 8 Isa 59:17;Efe 6:13-17 Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu. 9 1 The 1:10;2 The 2:14 Kwa kuwa Mungu hakutuweka ili tupate hasira yake, bali ili tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo; 10 1 The 4:14;Rum 14:8,9 ambaye alikufa kwa ajili yetu, ili tuishi pamoja naye, iwe tunakesha au tunalala. 11 Yud 1:20 Basi, farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake, hakika kama mnavyofanya.
12 1 Kor 16:18;1 Tim 5:17 Lakini, ndugu, tunataka mwatambue wale wanaojitaabisha kwa ajili yenu, na kuwasimamia ninyi katika Bwana, na kuwaonyeni; 13 mkawastahi sana katika upendo, kwa ajili ya kazi zao. Iweni na amani ninyi kwa ninyi.
14 2 The 3:6,11,15 Ndugu, tunawasihi, waonyeni wale wasiokaa kwa utaratibu; watieni moyo walio dhaifu; watieni nguvu wanyonge; vumilieni na watu wote. 15 Mit 20:22;Rum 12:17;1 Pet 3:9 Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.
16 Flp 4:4 Furahini siku zote; 17 Lk 18:1;Rum 12:12;Kol 4:2 ombeni bila kukoma; 18 Efe 5:20 shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu. 19 1 Kor 14:1,29,30,39 Msimzimishe Roho; 20 msitweze unabii; 21 1 Yoh 4:1 jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema; 22 Ayu 1:1,8;2:3 jitengeni na ubaya wa kila namna.
23 2 The 3:16 Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe muwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo. 24 1 Kor 1:9;2 The 3:3 Yeye ni mwaminifu ambaye awaita, naye atafanya.
25 2 The 3:1 Ndugu, tuombeeni. 26 1 Kor 16:20 Wasalimieni ndugu wote kwa busu takatifu. 27 Nawaapisha kwa Bwana, ndugu wote wasomewe waraka huu. 28 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi.