6 Basi tusilale usingizi kama wengine, bali tukeshe, na kuwa na kiasi. 7 Maana walalao usingizi hulala usiku, pia na walewao hulewa usiku. 8 Isa 59:17;Efe 6:13-17Lakini sisi tulio wa mchana, tuwe na kiasi, hali tukijivika kifuani imani na upendo, na chapeo yetu iwe tumaini la wokovu. 9 1 The 1:10;2 The 2:14Kwa kuwa Mungu hakutuweka ili tupate hasira yake, bali ili tupate wokovu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo;
Publicidade