1 Kum 17:6;19:15;Mt 18:16;1 Tim 5:19 Hii ndiyo mara yangu ya tatu kuja kwenu. Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa. 2 Nimetangulia kuwaambia; na, kama vile nilipokuwapo mara ya pili, vivyo hivyo sasa nisipokuwapo, nawaambia wazi wao waliotenda dhambi tangu hapo, na wengine wote, ya kwamba, nikija, sitahurumia; 3 kwa kuwa mnatafuta dalili ya Kristo, asemaye ndani yangu, ambaye si dhaifu kwenu, bali ana uweza ndani yenu. 4 Flp 2:7,8 Maana, alisulubiwa katika udhaifu, lakini anaishi kwa nguvu za Mungu. Maana sisi nasi tu dhaifu katika yeye; lakini tutaishi pamoja naye kwa uweza wa Mungu ulio kwenu. 5 1 Kor 11:28 Jichunguzeni wenyewe muone kama mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa iwe mmekataliwa. 6 Lakini natumaini kama mtajua ya kuwa sisi hatukukataliwa. 7 Nasi tunamwomba Mungu, msifanye lolote lililo baya; si kwamba sisi tuonekane tumekubaliwa, lakini ninyi mfanye lile lililo jema, ijapokuwa sisi tu kama waliokataliwa. 8 1 Kor 13:6 Maana hatuwezi kutenda neno lolote kinyume cha kweli, bali kwa ajili ya kweli. 9 Maana twafurahi, iwapo sisi tu dhaifu, nanyi mmekuwa hodari. Tena twaomba hili nalo, kutimilika kwenu. 10 2 Kor 2:3;10:8,11 Kwa sababu hiyo, naandika haya nikiwa mbali nanyi, ili, nikija, nisiwe na ukali wa kadiri ya uwezo ule niliopewa na Bwana, kwa kujenga wala si kwa kubomoa.
11 Flp 4:4;Rum 15:33 Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi. 12 1 Kor 16:20 Salimianeni kwa busu takatifu. Watakatifu wote wanawasalimu.
13 Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.