Salamu za mwisho na baraka
11 Flp 4:4;Rum 15:33Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi. 12 1 Kor 16:20Salimianeni kwa busu takatifu. Watakatifu wote wanawasalimu.
13 Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.