Manabii wa uongo na adhabu yao
1 Mt 24:11;1 Tim 4:1;Kum 13:1;Yud 1:4Lakini kulitokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia. 2 Isa 52:5Na wengi watafuata ufisadi wao; na kwa hao njia ya kweli itatukanwa. 3 Rum 16:18;2 Kor 9:5;1 The 2:5Na kwa tamaa yao watajipatia faida kwenu kwa maneno yaliyotungwa; wao ambao hukumu yao tangu zamani haikawii, wala maangamizi yao hayasinzii.